Mustakhbali wa watoto walioathirika na vita Syria lazima ulindwe: Ricky Martin

3 Juni 2016

Mwanamuziki nguli na balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Ricky Martin ametoa wito wa kuongeza juhudi za kulinda mustakhbali wa mamilioni ya watoto walioathirika na vita nchini Syria, ambao maisha yao yameghubikwa na ukimbizi wa ndani, machafuko na kutokuwa na fursa na maendeleo.

Wasyria takribani milioni 1.1 wamesaka hifadhi ya ukimbizi Lebanon tangu kuzuka kwa machafuko mwaka 2011 na zaidi ya nusu ya watu hao ni watoto. Watoto wakimbizi wako katika hatari ya kutumiwa na kunyanyaswa, huku idadi kubwa wakilazimika kufanya kazi badala ya kwenda shule.

Mwanamuziki huyo amesema ikiwa ni miaka sita ya vita vya Syria ambavyo vimeathiri maisha ya mamilioni ya watoto na familia zao, watoto milioni 2.8 hawako shuleni na wengi wakiwa ndio wanaofanya kazi hadi saa 12 kwa siku kukimu familia zao. Ameitaka dunia kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha watoto hawa wanalindwa na kuwawekea mazingira ambayo wanaweza kusoma na kuwezeshwa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter