Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mbegu na Pembejeo zasaidia wakimbizi Sudan Kusini

Mbegu na Pembejeo zasaidia wakimbizi Sudan Kusini

Watu 200,000 wakiwa ni wakimbizi na jamii zinazowapokea nchini Sudan Kusini wamepewa pembejeo za kilimo ikiwemo mbegu ili kuwasaidia kukabiliana na uhaba mkubwa wa chakula unaoikumba nchi hiyo.

Mradi huo umeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR na Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO ambayo yameungana ili kuwezesha wakimbizi na jamii zinazowapokea kujitegemea zaidi.

Taarifa iliyotolewa leo imeeleza kwamba tangu mwanzo wa mwaka huu, tani 186 za mbegu na pembejeo zimesambazwa kwenye majimbo ya Unity, Upper Nile, Jonglei, Central na Western Equatoria, wakati ambapo msimu wa kupanda mbegu ukiwa umeshaanza.

Tathmini iliyofanyika mwisho wa mwaka 2015 ilionyesha kiwango cha juu cha utapiamlo na utapiamlo wa kupindukia kwenye kambi za wakimbizi wa Upper Nile.

Usambazaji wa mbegu ni ufunguo, kwa mujibu wa FAO, ikitaja wakulima wanaoeleza kuwa hali ya njaa ikizidi, wakulima wengi hushindwa kubakiza mbegu kwa ajili ya msimu wa kilimo