Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zinazoendelea zachangia 90% za ukuaji wa uzalishaji bidhaa

Nchi zinazoendelea zachangia 90% za ukuaji wa uzalishaji bidhaa

Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda UNIDO inaonyesha kwamba nchi zinazoendelea na zinazoibuka zimechangia kwa asilimia 90 katika ukuaji wa uzalishaji wa bidhaa katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza ya mwaka 2016.

Kwa mujibu wa ripoti hii, ukuaji wa uzalishaji bidhaa umekuwa hafifu katika kipindi hiki, ukikuwa kwa asilimia 2.1 tu ikilinganisha na kipindi kile kile cha mwaka jana.

UNIDO imechambua zaidi ikieleza kwamba ukuaji huo umekuwa wa asilimia 0.3 katika nchi zenye uchumi ulioendelea, huku ukikuwa wa asilimia 4.6 kwenye nchi zinazoendelea.

Nchi iliyochangia zaidi ukuaji huo ni China.

Barani Afrika, uzalishaji bidhaa umepungua kwa asilimia 1.1, kutokana na upungufu wa mitaji na uuzaji wa bidhaa nje.

Kwa mujibu wa UNIDO, nchi zilizoendelea zinachangia kwa asilimia zaidi ya 60 katika uzalishaji bidhaa, huku uzalishaji wa bidhaa barani Afrika ukiwa ni asilimia 1.2 tu ya uzalishaji wote dunaini.