Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni jukumu la kila mtu kuhakikisha kuna mstakhbali wa kazi tunazotaka:ILO

Ni jukumu la kila mtu kuhakikisha kuna mstakhbali wa kazi tunazotaka:ILO

Ili mabadiliko mujarabu yapatikane katika mustakhbali wa kazi duniani, ni lazima kila mmoja achukue jukumu la kutekeleza mikataba ya kazi na kukubali mabadiliko.

Hayo yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani ILO Guy Ryder . Ameongeza kuwa kazi bora ni ufunguo wa kukabiliana na changamoto nyingi zinazomkabili mwanadamu hivi sasa.

Wawakilishi wa serikali, waajiri na wafanyakazi kutoka mataifa 187 nchi wanachama wanashiriki mkutano huo kujadili masuala mbalimbali ikiwemo kazi zenye hadhi kwa ajili ya amani, usalama na kukabili majanga katika nia ya kufikia ajenda ya 2030 ya malengongo ya maendeleo endelevu. Lawrence J. Johnson ni naibu mkurugenzi mkuu wa ILO kitengo cha utafiti

(SAUTI YA LAWRENCE)

"Tunachoangalia katika mustakhbali wa kazi ni vipi binadamu wataitumia teknolojia na jinsi teknolojia itakavyosaidia kutatua baadhi ya matatizo, duniani hivi sasa kuna watu bilioni saba na zaidi ya bilioni moja na nusu hawana kazi za kikidhi mahitaji yao, teknolojia inaweza kuwa suluhu."