Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Papa Francis kuzuru WFP katika kampeni ya kutokomeza njaa

Papa Francis kuzuru WFP katika kampeni ya kutokomeza njaa

Papa mtakatifu Francis atafanya ziara ya kwanza kwenye makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP mjini Roma mnamo Juni 13.

Hii ni ziara ya kwanza kabisa kufanywa na papa mtakatifu kwa WFP na inakuja wakati wa mwaka wa kwanza wa hatua za utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s. Malengo ambayo yameafikiwa nan chi wanachama wa Umoja wa mataifa kwa lengo la kushughulikia mizizi ya umasikini na njaa.

Kazi kubwa ya WFP ni kuhakikisha inafikia lengo la kutokomeza njaa ifikapo 2030. Akiwa WFP papa atawahutubia wajumbe wa bodi ya WFP ambao ni wawakilishi wan chi wanachama wa Umoja wa Mataifa na kisha atazungumza na wafanyakazi wa WFP.