Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yahofia Waeritrea kutimuliwa nchini Sudan

UNHCR yahofia Waeritrea kutimuliwa nchini Sudan

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limebaini kwa hofu kubwa hatua ya karibuni ya kuwatimua raia wa Eritrea walioko Sudan warejee Eritrea Mei 22. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Shirika hilo linasema takribani Waeritrea 313 walikamatwa Mei 6 kwenye mji wa Dongola Kaskazini mwa Sudan.

Walifikishwa mahakamani ,kuhukumiwa na kukutwa na hatia ya kuingia Sudan kwa njia haramu chini ya sheria za kimataifa za uhamiaji na walilazimishwa kurejea nyumbani.

Nora Sturm ni msemaji wa UNHCR, Geneva

Sita kati yao walitambuliwa kuwa ni wakimbizi, na wengine hawakuwa wameomba hifadhi lakini ni vigumu kufahamu iwapo walipatiwa fursa ya kufanya hivyo.”

UNHCR inasema hiyo si mara ya kwanza kwani kabla ya Mei 22 raia wengine 129 wa Eritrea walikmatwa na kurejeshwa kwa nguvu nchini mwao.

UNHCR inasema kuwarejesha kwa nguvu wakimbizi, waomba hifadhi au watu wanaohitaji ulinzi ni kinyume cha sheria za Sudan na mkataba wa kimataifa wa wakimbizi wa 1951