Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada waingia Daraya kwa mara ya kwanza baada ya miaka 4:

Msaada waingia Daraya kwa mara ya kwanza baada ya miaka 4:

Msafara wa misaada umeingia katika eneo linalozingirwa la mji wa Daraya nchini Syria kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2012 shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA nchini Syria.

Video inayoonyesha magari ya Umoja wa mataifa nay ale ya shirika la mwezi mwekundu la nchi za Kiarabu yakiingia mjini humo imechapishwa Jumatano.

Baadhi ya misaada iliyowasili ni maziwa ya watoto, dawa, chanjo na vifaa vya lishe limesema shirika la OCHA.

Chakula pia kiliwasili mapema kwenye eneo la Moademiah nje ya mji mkuu Damascus kwa kutumia msafara huo huo.