Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwawezesha wanawake kunasaidia kutokomeza umasikini: Puri

Kuwawezesha wanawake kunasaidia kutokomeza umasikini: Puri

Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women kimesisitiza umuhimu wa kuhusisha suala la usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake katika jitihada za kutokomeza umasikini kwenye nchi zenye maendeleo duni (LDC’s).

Akizungumza kwenye hitimisho la mkutano wa tathimini ya nchi zenye maendeleo duni mjini Antalya Uturuki, naibu mkurugenzi mtendaji wa UN Women Bi Lakshmi Puri amesema kuna uhusiano mkubwa baina ya usawa wa kijinsia , uwezeshaji wanawake na kutokomeza umasikini.

(SAUTI YA LAKSHIMI PURI)

“Kutokuwepo usawa wa kijinsia, ubaguzi na ukatili dhidi ya wanawake vinachagiza umasikini, na kutumbukia katika umasikini, hivyo tutahitaji kuwa na mzunguko mzuri badala ya mzunguko wenye madhara uliopo katika nchi za LDC’s”.