Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OHCHR: yakasirishwa na Iran kucharaza viboko baada ya sherehe za mahafali

OHCHR: yakasirishwa na Iran kucharaza viboko baada ya sherehe za mahafali

Nchini Iran uamuzi wa kuwacharaza bakora wanafunzi 35 baada ya kufanya sherehe za maafali umelaaniwa vikali na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa Rupert Colville msemaji wa ofisi hiyo , adhabu hiyo inaaminika kutolewa kwa sababu wakulikuwa na mchanganyiko wa wanawake na wanaume kwenye maafali hayo mjini Qazvin , Kaskazini mwa Tehran na wengine hawakuwa wamevaa hijab.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

"Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali , wanafunzi hao walikamatwa Alhamisi, wakahojiwa na kuhukumiwa na ofisi ya mwendesha mashitaka viboko 99 kila mmoja na kisha wakacharazwa bakora wote ndani ya saa 24”.

Ofisi ya haki za binadamu inasema sehemu zingine nchini Iran kumearifiwa kutumika bakora dhidi ya mwanamke anayekuwa na mahusiano ya ngono nje ya ndoa.

Mwaka jana Zaidi ya watu 400 waliripotiwa kucharazwa bakora kwa kutofunga wakati wa Ramadhan ingawa serikali inakanusha idadi hiyo.