Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tukiwatelekeza wakulima wadogo wadogo tunatelekeza mustakhbali wetu:IFAD

Tukiwatelekeza wakulima wadogo wadogo tunatelekeza mustakhbali wetu:IFAD

Kukiwa na takribani watu milioni 795 wanaokabiliwa na njaa duniani na wengine milioni 60 wanaohitaji msaada wa chakula kutokana na ukame na mavuno hafifu yaliyopsababishwa na El Niño, mawaziri wa kilimo kutoma mataifa ya G-20 wanaokutana China wanakabiliwa na kibarua kigumu, amesema Rais wa wa shirika la Umoja wa mataifa lililojikita kusaidia wakulima wadogo wadogo.

Kwa mujibu wa Kanayo Nwanze Rais wa mfuko wa Umoja wa mataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD mkutano huu wa nmawaziri wa G-2- umekuja wakati muafaka, kwani sasa ni muhimu kuliko wakati mwingine wowote kuwekeza kwa wakulima wadogowadogo , ili kuwajengea uwezo wa kukabiliana na misukosuko inayosababisha mavuno hafifu.

Ameongeza kuwa wakulima hao ndio uti wa mgongo wa mfumo wa chakula duniani na endapo tunatawatelekeza basi tunatelekeza mustakhbali wetu.

Zaidi ya watu bilioni tatu karibu nusu ya watu wote duniani wanaishi vijijini na wengi wao wanategemea kilimo kwa ajili kuishi na kipato pia.