Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kubadili nchi au kusitisha Olimpiki sio muarubaini: WHO

Kubadili nchi au kusitisha Olimpiki sio muarubaini: WHO

Tukisalia katika afya ,Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema tathimini ya sasa inaonyesha kuwa kusitisha au kubadili eneo la kufanyia mashindano ya Olimipiki hakutaleta mabadiliko makubwa katika kudhibiti kuenea kwa virusi vya Zika duniani . Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(TAARIFA YA PRISCILLA)

Brazil ambayo ni mwenyeji wa mashindano hayo ni miongoni mwa nchi ambazo hadi sasa zinaripoti maambukizi ya Zika yanayoenenezwa na mbu.

WHO imesema katika taarifa yake kuwa  kutokana na ukweli kwamba bado watu husafiri katika nchi hizo kwasababu tofauti,  njia bora ya kupunguza hatari ya ugonjwa ni kufuata kanuni za kiafya za kusafiri.

Tarik Jasarevic ni msemeji wa WHO.

(SAUTI RATIK)

‘‘Tathimini binafsi ya hatari ya kiafya na hii inaongozwa na mfumo mzima wa hatua za kinga na ulinzi. Hii inajumuisha mamlaka inayotakiwa kuhakikisha  mazingira yako salama kadri inavyowezekana.’’