Skip to main content

MONUSCO na FARDC wahakikishe usalama kwa wakazi wa Lubero: Djinnit

MONUSCO na FARDC wahakikishe usalama kwa wakazi wa Lubero: Djinnit

Jamii ya eneo la Lubero, Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inahitaji hasa usalama, na hilo ni jukumu na jeshi la kitaifa kwa ushirikiano na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO.

Hayo amesema Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukanda wa maziwa makuu, Said Djinnit, akiwa ziarani mashariki mwa DRC ambapo amejadiliana na wananchi na kusikiliza matarajio yao.

Kwenye video iliyotolewa na MONUSCO, Bwana Djinnit ameeleza kwamba mahitaji ni mengi, yakiwa ni ajira, maelewano baina ya makabila, ushirikishwaji wa vijana kwenye jamii, lakini hasa usalama akisema

(Sauti ya Bwana Djinnit)

“Jitihada zinafanyika lakini bado kuna mengi ya kufanya. Tumekutana na jamii ya eneo hilo. Tumefurahi kuona kwamba wameridhishwa na mafanikio ya ushirikiano baina ya jeshi la kitaifa na MONUSCO, lakini wanataka vikosi hivyo viongeze bidi, na ndivyo tunavyotaka pia sisi wadhamini ”