Skip to main content

Walinda amani wazungumzia wanayokumbana nayo kila uchao #Peacekeepingday

Walinda amani wazungumzia wanayokumbana nayo kila uchao #Peacekeepingday

Mei 29 kila mwaka,  hufanyika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa. Siku hii huaadhimishwa ili kuwakumbuka wale waliopoteza maisha yako wakilinda amani na pia kutoa heshima kwa ujasiri wa wanaofanya kazi hiyo. Tangu kuanzishwa kwa misheni ya kwanza ya ulinzi wa amani mwaka 1948 mpaka Aprili 2016, wanajeshi, polisi na wafanyakazi 3,400 wamepoteza maisha katika ajali, migogoro na magonjwa.

Hivi sasa, kuna zaidi ya walinda amani askari na polisi 105,000  kutoka nchi wanachama 124 wa Umoja wa Mataia. Barani Afrika, walinda amani wanatoka Ethiopia, Rwanda, Senegal, Burkina Faso, Ghana, Tanzania, Kenya na Uganda. Basi ungana nami Assumpta Massoi kwenye Jarida hili maalum likiangazia majukumu yao ya kila siku,  ikiwemo changamoto kuanzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hadi Darfur, Sudan.