Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi nyingi za LDCs hazijafuzu vigezo: Chandra

Nchi nyingi za LDCs hazijafuzu vigezo: Chandra

Nchi nyingi zilizo na maendeleo duni LDCs hazijafuzu kigezo cha kuondolewa katika kundi hilo amesema Gyan Chandra Acharya msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na nchi hizo.

Akiongea jumamosi wakati wa mkutano unaoendelea mjini Antalya Uturuki ukiangazia utekelezaji wa mkakati wa maendeleo wa mwaka 2011 (IPOA) uliofikiwa mjini Istanbul amesema ni nchi 12 kati ya 48 zilizofikia asilimia saba ya malengo.

Hivyo amesisitiza.

(SAUTI ACHARYA)

''Wazo letu lakuwa na mkutano huu wa kimataifa ni kusongesha mchakato. Ikiwa tunafanikisha malengo tunayaendelezaje, kama hatuyafikii, tunawezaje kuyaharakisha zaidi kuliko ambavyo imekuwa kwa miaka mitano iliyopita.''

 Amekariri umuhimu wa kuwa na uongozi thabiti wa kitaifa na usaidizi thabiti wa kimataifa.

Kwa upande wake mratibu wa asasi y akimataifa ya kufuatiia nchi hizi  LDC Watch, Gauri Pradhan,  amewakilisha waraka wa asasi za kiraia akisema.

 (SAUTI GAURI)

‘‘Wawakilishi wa asasi za kiraia kutoka sehemu mbalimbali duniani, kutoka LDCs wamekuwa na majadiliano thabiti kuhusu masuala kadhaa, tunajaribu kutafakari waraka wa matokeo na kupatia asasi hizi mitazamo na kukusanya sauti kutoka mashinani”