Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya wahamiaji haramu waliorejeshwa Burundi kutoka Rwanda

Hali ya wahamiaji haramu waliorejeshwa Burundi kutoka Rwanda

Mapema mwezi huu wa Mei, serikali ya Rwanda iliamua kufurusha raia wapatao 2,000 wa Burundi waliokuwa wakiishi nchini humo bila vibali. Warundi hao wamevuka mpaka na kuwasili kwenye jimbo la Kirundo kaskazini mwa Burundi linalopakana na Rwanda ambapo wamepewa hifadhi na familia za wakazi wa eneo hilo na misaada ya msingi na serikali za mitaa.

Wakati huo huo mashirika ya kimataifa ya kibinadamu yamekuwa yakitathmini hali yao na kuandaa mpango wa msaada wa dharura kwa ajili ya kuwapelekea misaada ya chakula na vifaa vingine, huko Shirika la Kimataifa la Uhamiaji(IOM) likiripoti kuwa wahamiaji kahaa wanaendelea kuwasili mpakani kila siku.