Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya wahamiaji 200,000 wawasili Ulaya mwaka 2016

Zaidi ya wahamiaji 200,000 wawasili Ulaya mwaka 2016

Idadi ya wahamiaji na wakimbizi waliowasili Ulaya kwa njia ya boti katika kipindi cha miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2016 imefika zaidi ya 200,000.

Idadi hiyo kwa mujibu wa takwimu za shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM, ni maradufu ya idadi ya mwaka uliopita. Wahamiaji hao wamevuka bahari ya Mediterania na kufika Ulaya kupitia Italia, Ugiriki, Cyprus na Hispania, viashiria vikionyesha kuwa wahamiaji zaidi wanawasili Ugiriki, huku idadi ya wanaowasili kupitia Italia ikipungua.

Joel Millman ni msemaji wa IOM.

(Sauti ya Bwana Millman)

"Idadi ya vifo niliyoripoti siku ya jumanne ilikuwa ya chini sana kwa mwezi wa Mei, lakini sasa siyo ya chini sana tena kwa sababu kwa kipindi cha saa 24 zilizopita, kumekuwa angalau ajali tatu kwenye Bahari ya Mediteranea ambazo zitafanya mwezi Mei, badala ya kuwa mwezi wenye idadi ndogo ya vifo katika historia ya hivi karibuni, sasa kwa bahati mbaya sasa umekuwa mwezi wenye vifo vingi.”