Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa LDCs wazinduliwa Uturuki, Tanzania yaangaziwa

Mkutano wa LDCs wazinduliwa Uturuki, Tanzania yaangaziwa

Wawakilishi wa jamii ya kimataifa na nchi 48 zilizoorodheshwa kuwa na maendeleo duni (LDCs) wameanza leo mjini Antalya Uturuki mkutano wa kimataifa kwa ajili ya tathmini ya mpango kazi wao.

Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Lengo la mkutano huo ni kuangazia mafanikio ya nchi hizo katika kutokomeza umaskini, kuendeleza maendeleo ya kijamii na kudumisha ukuaji wa uchumi, hadi hatimaye nchi hizo ziondolewe kwenye orodha ya LDCs.

Ujumbe wa Tanzaniai kwenye mkutano huo wa siku mbili unaongozwa na Mwakilishi wake wa Kudumu kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Uswisi, Balozi Modest Mero anayesema lengo pia ni kutathmini utekelezaji wa mpango kazi kwa LDCs uliopitishwa mwaka 2011.

(Sauti ya Bwana Mero)

Moja ya malengo ya mpango kazi kwa LDCs ni kuhakikisha kwamba nusu ya nchi 48 zenye maendeleo duni zinafikia kiwango cha kutokuwa LDCs tena ifikapo mwaka 2020.

Hadi leo ni nchi nne tu ambazo zimeondolewa kwenye orodha hiyo, zikiwa ni Samoa, Botswana, Cape Verde na Maldives.