Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ubia wa kimataifa wahitajika kwa mazingira: Eliasson

Ubia wa kimataifa wahitajika kwa mazingira: Eliasson

Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson wa Umoja wa Mataifa, amesema kutunza mazingira ni msingi wa amani, maendeleo na utu kwa wote.

Amesema hayo akihutubia mkutano wa pili wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEA, linalofanyika wiki hii huko Nairobi, Kenya.

Bwana Eliasson ameongeza kwamba ni lazima kuchukua hatua mapema na kwa ushirikiano, ili kudhibiti madhara ya mabadiliko ya tabianchi, akizingatia umuhimu wa ubia wa kimataifa.

(Sauti ya Bwana Eliasson)

Kuachana na mafuta ya petroli au kisukuku kutakuwa vigumu hata kama sote tunajua kwamba suluhu mbadala zipo. Bado kuna fikra duni kwamba tunapaswa kuchagua baina ya ukuaji wa uchumi na utunzaji wa mazingira. Ni vigumu kuachana na mazoea na maslahi yenye nguvu hayaachwi kwa ridhaa. ”

 

Kwa upande wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema Afrika ndio bara linaloweza kunufaika zaidi kutokana na juhudi za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, akitumai nchi nyingi zaidi zitapatia kipaumbele suala hilo.