Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO na wapishi maarufu watoa kitabu kuhusu vyakula vya jamii ya kunde

FAO na wapishi maarufu watoa kitabu kuhusu vyakula vya jamii ya kunde

Je, wapenda maharage, choroko, dengu na aina zingine za kunde? Basi utafurahia habari kuwa, Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) limezindua leo kitabu kinachoangazia mapishi na faida za vyakula hivyo vya jamii ya kunde. Taarifa kamili na Assumpta Massoi

(Taarifa ya Assumpta)

Kitabu hicho cha kurasa 190, kimesheheni ustadi wa mapishi ya vyakula vya jamii ya kunde kutoka kwa wapishi kumi mashuhuri duniani.

Kitabu hicho kinatoa maelezo kuhusu faida za vyakula vya jamii ya kunde kwa lishe, afya, bayo anuai na uhakika wa kuwa na chakula.

Aidha, kinaeleza hatua kwa hatua ni vitu gani unavyopaswa kuzingatia unaponunua vyakula hivyo, jinsi ya kuvikuza nyumbani na jinsi ya kuvipika. Sile (Shila) Obroin, ni mmoja wa maafisa wa FAO walioratibu na kuhariri kitabu hicho

Vyakula vya jamii ya kunde ni miongoni mwa vyakula vyenye kiwango cha juu zaidi cha lishe, kwa sababu vina kiwango maradufu cha protini kinachopatikana katika ngano na mara tatu ya kile cha mchele. Vina mafuta kidogo, vimejaa madini ya potasiamu, magnesi na vinasaidia mfumo wa kusagisha chakula tumboni. Havina lehemu, na gluten. Katika kilimo, vinaongeza rutuba katika udongo.”