Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nina matarajio makubwa na mkutano wa LDCS- Acharya

Nina matarajio makubwa na mkutano wa LDCS- Acharya

Mkutano wa nchi zenye maendeleo duni, LDCs ukitarajiwa kuanza kesho huko Antalya, Uturuki, msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na nchi hizo Gyan Chandra Acharya amesema ana matarajio makubwa kutokana na mijadala itakayohusisha mawaziri, nchi hisani na mashirika ya kiraia. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa huko Antalya, Bwana Acharya amesema..

(Sauti ya Acharya-1)

“Tutakuwa na mawazo thabiti kuhusu wapi LDCs zimepata mafanikio, wapi bado zinapata changamoto na wapi jamii ya kimataifa isaidie zaidi na zenyewe zifanye nini zaidi.”

Halikadhalika akagusia nyaraka inayotarajiwa kupitishwa mwishoni mwa mkutano inapendekeza..

(Sauti ya Acharya-2)

“ODA ambayo ni misaada rasmi ya maendeleo inayoelekezwa kwa nchi zenye maendeleo duni itaimarishwa.”