Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hospitali zazidi kulengwa na mashambulizi : WHO

Hospitali zazidi kulengwa na mashambulizi : WHO

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO imebaini kuwa mashambulizi takriban 600 yamelenga wauguzi ulimwenguni kote mwaka 2014 na 2015 na kusababisha vifo zaidi ya 900.

Utafiti huo umefanyika kwenye nchi 19 tu ambapo takwimu zilikuwa zinapatikana ambapo Syria ndio inashika nafasi ya kwanza kwa kuwa na mashmbulizi zaidi ikifuatiwa na Ukanda wa Gaza na ya tatu Iraq..

Rick Brennan ni mkurugenzi wa WHO wa idara ya masuala ya dharura .

(Sauti ya Brennan)

"Huenda moja ya matokeo ya ripoti yanayotia wasiwasi zaidi ni kwamba karibu theluthi mbili ya mashambulizi dhidi ya huduma za afya, vituo vya afya, wauguzi, magari ya wagonjwa na wagonjwa yamekuwa makusudi."