Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twahitaji hatua za kimkakati kulinda mazingira- Glasser, Steiner

Twahitaji hatua za kimkakati kulinda mazingira- Glasser, Steiner

Wakati huu ni zama za kubadili uhusiano wetu na sayari ya dunia tunamoishi ili kupunguza athari za uharibifu wa mazingira.

Hiyo ni sehemu ya tahariri iliyochapishwa kwenye gazeti ya Huffington Post na Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu udhibiti wa majanga, Robert Glasser na mkuu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa Achim Steiner.

Wamesema sasa ni lazima kuchukua hatua za kimkakati na si za muda mfupi na mabadiliko yanayopaswa kufanyika yanatokana na uharibifu ambao umefanywa na binadamu.

Glasser na Steiner wametaja hatua za kuchukua kuwa ni pamoja na kuweka mifumo ya tahadhari dhidi ya majanga, kuweka kanuni kali kwenye mipango miji, kusimamia kanuni za ujenzi na kuweka hatua za kuhifadhi mazingira.

Wamekaribisha hatua iliyotangazwa na Japan kwenye kikao cha kundi la nchi saba tajiri zaidi duniani, G7 la kujumuisha kwa mara ya kwanza ajenda ya suala la kupunguza athari za majanga.