Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna hatari ya watu kunyongwa hadharani Gaza umeonya UM

Kuna hatari ya watu kunyongwa hadharani Gaza umeonya UM

Ikizungumzia taarifa ya uongozi wa Gaza kwamba kuna idadi ya watu watanyongwa, Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetoa taarifa ya kukumbusha kwamba hukumu za kifo zinaweza kutumika tu ambapo viwango vya haki vimetumika katika kesi.

Ofisi hiyo pia imesema kuwanyoka watu hadharani ni haramu chini ya sheria za kimataifa. Tangazo hilo la uongozi wa Gaza linasema watu 13 watanyongwa kufuatia wito wa familia za watu waliowauwa.

Ofisi ya haki za binadamu inasema inatiwa hofu na hali hiyo na ina mashaka endapo viwango vya haki vinavyostahili katika kesi kama vimefikiwa.

Pia ina hofia taarifa kwamba hukumu hiyo itatekelezwa bila idhini ya Rais Mahmoud Abass kufuatia kutiwa saini na bunge la nchi hiyo.