Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama laiondolea vikwazo Liberia

Baraza la usalama laiondolea vikwazo Liberia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo kwa kauli moja limepitisha azimio la kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Liberia hatua iliyotafsiriwa kama matokeo ya kufanya kazi pamoja.

Vikwazo hivyo viliwekwa mwaka 2003 kufuatia vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Akilihutubia baraza hilo muda mfupi baada ya kuondolewa kwa vikwazo, mwakilishi maalum wa Marekani katika ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kisiasa David Pressman amesema hii ni hatu amuhimu.

( SAUTI PRESSMAN)

‘‘Huu ulikuwa ushuhuda wa kile kinachoweza kufikiwa pale ambapo vikwazo vinawekwa kwa lengo, na kwa mikakati ya kukuza amani ya kimataifa na usalama na kuchagizwa na maendeleo ya kisiasa kutoka serikalini.’’

Kuhusu kile kinachopaswa kufanywa sasa na serikali ya Liberia...

( SAUTI PRESSMAN)

‘Ili Liberia ilinde mafaniko yaliyopatikaana kwa miaka 12, tunaisisitiza serikali kutoa kipaumbele katika kujengea uwezo sekta ya usalama na kuendeleza uwezo wa wakala wake wa usalama ili kusimamia vyema uingizwaji wa silaha, kuweka alama silaha na doria mipakani.’’