Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yalaani shambulio lililouwa 11 Kabul

UNAMA yalaani shambulio lililouwa 11 Kabul

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) umelaani shambulio la bomu nje ya mji wa Kabul ambalo limesababisha vifo vya watu 11 na kujeruhi 10.

Kwa mujibu wa taarifa ya UNAMA mlipuaji alilipua basi la wafanyakazi wa mahakama ya jimbo liitwalo Wardak ambapo pia shamulio jingine mjini Kabul limesababaisha vifo vya abiria katika basi na watu waliokuwa wamesimama katika eneo hilo wakiwamo watoto sita.

Tangu mwezi Januari mwaka huu, UNAMA imethibitisha mashambulio 14 tofauti, yakiwalenga mahakimu, waendesha mashtaka na maafisa wa mahakama na kusababisha vifo vya watu tisa na kujeruhi wengine 19.

Kadhalika ujumbe huo umethibitisha matukio manne ya utekwaji wa wafanyakazi wa mahakama. Kundi la wanamgambo wa Taliban limekiri kuhusika na mashambulio saba.

Mkuu wa UNAMA Nicholas Haysom amesema kuwa mashambulio dhidi ya mamlaka za mahakama ni ya uwoga na kinyume na sheria za kimataifa za kibinadamu.