Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi ya ulinzi wa amani ni zaidi ya kazi ya polisi na askari jeshi- Elizabeth Mgaya Nebo

Kazi ya ulinzi wa amani ni zaidi ya kazi ya polisi na askari jeshi- Elizabeth Mgaya Nebo

Kwa mtu aliye nje ya mfumo wa Umoja wa Mataifa,  huenda ikawa ni vigumu kidogo kufahamu kuwa kazi ya ulinzi wa amani  ni zaidi ya kazi ya askari jeshi na askari polisi.

Kuelekea siku ya walinda amani duniani mwaka huu,  mnamo tarehe 29 Mei,  tunakutana na watu mbali mbali wanaojishughulisha na operesheni za ulinzi wa amani,  ingawa wao sio wanajeshi au askari polisi.

Mwenzetu Jumbe Omari Jumbe amekuwa akizungumza na Elizabeth Mgaya Nebo, kutoka Tanzania, ambaye anafanya kazi kwenye kitengo cha siasa, katika Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, Sudan (UNAMID).

(Sauti ya Elizabeth Mgaya Nebo)