Skip to main content

FAO na WFP wasaidia familia za CAR kukabiliana na msimu wa mwambo

FAO na WFP wasaidia familia za CAR kukabiliana na msimu wa mwambo

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR,  familia zipatazo 50,000  zilizoathirika na njaa  zimeanza kupewa msaada wa chakula na mbegu  wakati msimu wa mwambo ukikumba wakulima.

Taarifa ya Shirika la Chakula na Kilimo FAO imeeleza kwamba FAO inatoa mbegu na vifaa vya kilimo, huku Shirika la Mpango wa Chakula WFP likisambaza mahindi, mchele, karanga na maharage kwa familia hizo hizo ili  wasianze kula mbegu zao na kushindwa kuanza kulima.

Roberta Canulla ni afisa wa FAO.

(sauti ya Roberta)

« Asilimia 75 ya idadi ya watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanategemea kilimo kwa chakula na kipato. Kwa hiyo sekta ya kilimo ni msingi kwa maendeleo na mustakhabali wa nchi na yenye fursa kubwa zaidi kwa ukuaji wa uchumi na kwa vijana na wazee. »