Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuchagua amani ni rahisi kuliko kulipiza kisasi:Ochen

Kuchagua amani ni rahisi kuliko kulipiza kisasi:Ochen

Watoto na vijana wanaoishi kwenye kambi za wakimbizi na  hata wakimbizi wa ndani kila mahali wako katika hatari ya kuuawa, kutekwa au hata kujeruhiwa na wanaishi kwa wasiwasi hata wa kupata mlo. Flora Nducha na taarifa zaidi.

(TAARIFA YA FLORA)

Hayo yamesemwa na kijana Victor Ochen , aliyekuwa askari mtoto wa zamani kwa miaka 20 huko Kaskazini mwa Uganda.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na migogoro ya vita amesema baadhi ya rafiki zake waliamua kubeba silaha na kulipiza kisasi kwa kushirikishwa jeshini ili lakini yeye akakataa kubeba silaha na kuchagua amani badala yake.

(SAUTI VICTOR OCHEN)

"Uponyaji ni njia pekee ya kuweza kusonga mbele, nilipoangalia hakukuwa na njia nyingine nikasema: sikubali kujifunga katika mateso yangu mwenyewe na hisia za kushindwa. Nilipokuwa mtoto nilisema sitaki kuishi maisha haya nilinayoishi, na hiyo ilikuwa amani.”

Victor hivi sasa anasaidia watoto wengine kupitia mradi wa mtandao wa vijana barani Afrika.