Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yataja washindi wa tuzo ya elimu kwa wasichana na wanawake

UNESCO yataja washindi wa tuzo ya elimu kwa wasichana na wanawake

Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu, sanyansi na utamaduni UNESCO Bi Irina Bokova ametangaza majina ya washindi wawili wa tuzo ya nobeli, ambayo ni ya kwanza ya UNESCO kwa ajili ya elimu ya wasichana na wanawake.

Washidi hao wawili ni Kurugenzi ya elimu ya utotoni ya wizara ya elimu na Utamaduni kutoka Jamhuri ya Indonesia na mwanafunzi wa kike wa Network Trust kutoka Zimbabwe, ambao wametambuliwa kwa ajili ya miradi yao ya ubunifu.

Kurugenzi ya elimu ya Jarkata Indonesia inatunzwa kwa mradi wake wa Kuboresha upatikanaji na ubora wa elimu ya wasichasna kupitia elimu ya utotoni na masuala ya jinsia katika jamii. Inahusisha wasichana kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka minane kwa lengo la kuwapa fursa za elimu na usawa wa kijinsia.

Naye mwanafunzi kutoka Harare Zimbabwe anatunzwa kwa mradi wake wa uwezeshaji wa elimu ya Juu kwa wanafunzi wanawake kupitia maendeleo ya uongozi na mipango uelimishaji. Washindi hao kila mmoja atatunikiwa dola 50,000 wakati wa hafla maalumu itakayofanyika Beijing Uchina kwenye semaina ya kimataifa ya elimu kwa wasichana na wanawake kuanzia Juni 4 hadi 7. Tuzo hiyo inafadhiliwa na serikali ya China.