Skip to main content

Mazingira na afya ni masuala mtambuka, tushiriki sote- UNFCCC

Mazingira na afya ni masuala mtambuka, tushiriki sote- UNFCCC

Katibu mkuu mtendaji wa mkataba wa Umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabia nchi (UNFCCC). Christiana Figueres, amesisitiza uzingatiaji wa uhusiano kati ya mabadiliko ya tabianchi na afya kama njia mojawapo ya kudhibiti magonjwa.

Bi. Figueres amesema hayo mbele ya Baraza la shirika la afya duniani, WHO huko Geneva, Uswisi, baada ya washiriki kuelezwa umuhimu wa sekta mbali mbali kushirikiana ili kufanikisha malengo yahusianayo na afya katika ajenda 2030 au SDGs.

Amesema harakati za kuimarisha afya hivi sasa zimejikita kwenye matibabu lakini ni vyema kubadili mwelekeo hasa wa kudhibiti mazingira la sivyo katika miaka mitano ijayo anga litakuwa limeharibiwa na madhara yake kiafya yatudumu miongo na miongo.

Katika mkutano huo, washiriki wamekubaliana kuimarisha mifumo ya afya ya kitaifa ili huduma ya afya iwe kwa wote kama njia mojawapo ya kufanikisha SDGs.