Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujangili ni hatari kwa mazingira na chachu ya migogoro: UNODC

Ujangili ni hatari kwa mazingira na chachu ya migogoro: UNODC

Ujangili wa wanyama pori na biashara haramu ya viumbe sio tu ni hatari kwa mazingira bali pia ni chachu ya migogoro.

Hayo ni kwa mujibu wa tathimini ya kwanza ya kimataifa kuhusu uhalifu dhidi ya wanyama pori iliyochapishwa Jumanne na ofisi ya Umoja wa mataifa ya madawa na uhalifu UNODC.

Ripoti ya kimataifa ya uhalifu dhidi ya wanayama pori inatoa wito wa kuchukua jukumu kwa pamoja kukabiliana na ilichokiita changamoto ya kimataifa.Ripoti hiyo inaonyesha jinsi makundi ya uhalifu wa kimataifa wanavyojihusihsa katika biashara hii kutokana na takwimu zinazoainisha kukamatwa katika mataifa 120 bidhaa haramu za wanyama pori.

Hata hivyo waandishi wa ripoti wanasema ni vigumu kupata jumla kamili ya fedha zinazopatikana na biashara hiyo haramu. Ripoti hiyo imetoa wito wa kuchukuliwa hatua za pamoja kuziba pengo katika sheria, vyombo vya dola na mfumo wa haki na uhalifu kupunguza athari za usafirishaji haramu wa wanyama pori.