Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Boko Haramu inaendelea kuwaweka roho juu wananchi Nigeria:WHS

Boko Haramu inaendelea kuwaweka roho juu wananchi Nigeria:WHS

Kundi la Boko Haramu ambalo linalaumiwa kwa ukatili, mauaji na vitendo vya kigaidi linaendelea kuziweka jamii roho juu katika maeneo mbalimbali nchini Nigeria likiwemo jimbo la Adamawa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria ambako watu wanafungasha virago kila uchao kwa sababu ya kundi hilo.

Aishatu Marginal mwenye umri wa miaka 59, ni muuguzi mstaafu,amekuwa Istanbul Uturuki kwenye mkutano wa dunia wa masuala ya kibinadamu kuwakilisha jamii iliyoathirika na Boko Haramu.

Binafsi amesaidia kuwapa hifadhi zaidi ya wakimbizi wa ndani 50 kwa muda wa miezi saba. Ilikuwaje?

(SAUTI YA AISHATU CUT-1)

"Walikuja nyumbani kwangu wakiwa na hali mbaya nisingeweza kuwakataa, wengi wanawake na watoto walikuwa wamechoka sana ikanibidi kuwapokea. Wakakaa kwa miezi saba, haikuwa rahidi lakini kwa neema ya mungu na msaada wa majirani tunaweza. Wanalala nyumbani kwangu, wanakula nyumbani kwangu, na kila siku nanunua dawa kwa ajili ya watoto

Na baada ya mkutano huo wa Istanbull anaeleza matumaini yake."

(SAUTI AISHATU -2)

"Tunatumai kutakuwa na uwajibikaji zaidi wa kuwasaidia wakimbizi wote wa ndani walio kambini na wanaohifadhiwa kwenye jamii, na mwishowe tunatumai mapambano haya yatakwisha, ulinzi na usalama kupatikana kwa watu wote walioathirika Kaskazini Mashariki mwa Nigeria."