Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushirika mpya umezinduliwa leo ukilenga maandalizi dhidi ya majanga:WHS

Ushirika mpya umezinduliwa leo ukilenga maandalizi dhidi ya majanga:WHS

Ushirika mkubwa mpya umezinduliwa leo kwenye hitimosho la mkutano wa dunia wa kibinadamu kwa minajili ya nchi na jamii kujiandaa vyema kwa ajili ya majanga , wakati dunia ikiungana kukabilia dharura za kibinadamu.

Ushirika huo (GPP) unaongozwa na Vulnerable Twenty au (V20 ) kundi la mawaziri wa fedha wa kongamano la mazingira magumu ambalo linawakilisha mataifa yanayoendelea 43 yaliyo katika hatari, kwa ushirikiano na mashirika ya Umoja wa mataifa likiwemo la chakula na kilimo FAO, ofisi ya Umoja wa mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA, shirika la mpango wa chakula duniani WFP pamoja na kitengo cha kimataifa cha Benki ya dunia cha upunguzaji wa majanga na ujenzi mpya (GFDRR).

image
Ugawaji wa chakula Aleppo, Syria.(Picha:OCHA/Gemma Connell)
Ushirika huo mpya utaimarisha uwezo wa kujiandaa mapema katika nchi 20 ili ziweze kufikia kiwango cha chini cha utayari ifikapo mwaka 2020 kwa ajili ya hatari ya baadaye ya maafa hasa itakayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Mwakilishi wa V20 Roberto B.Tan amesema , lengo la ushirika huo na jumuiya ya kimataifa ni kuhakikisha kwamba wakati janga linatokea mppango na usaidizi vipo tayari ili watu waweze kurejea katika maisha ya kawaida haraka iwezekanavyo.

image
Helen Clark.(Picha:UM/NICA:604020)
Kwa upande wake mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP Helen Clark amesema Ushirika huu utazisaidia nchi kufikia kiwango ckinachoridhisha cha maandalizi dhidi ya majanga na dharura zingine, kwa nia ya kuokoa maisha , kulinda maendeleo, na kupunguza athari.
image
Stephen O'Brien.(Picha:UM/Mark Garten)
Akisistiza kwamba majanga na dharura zingine zisiwe Zahma kubwa ya kibinadamu kama maandalizi yanayostahili yatakuwepo, mkuu wa OCHa Stephen O’Brien amesema , ushirika huo unatoa fursa ya maandalizi muafaka na kuepuka zahma kubwa.
image
Laura Tuck.(Picha:World Bank)
Laura Tuck kutoka Bank ya Dunia amesema wanaungana na mashirika ya Umoja wa Mataifa kuunga mkono ushirika huu kwa sababu ya kusaidia kujenga uimara wa taasisi za kitaifa na kijamii na kuhakikisha mipango na ufadhili wa majanga ni sehemu ya mifungo ya nchi ya udhibiti majanga.
image
José Graziano da Silva.(Picha:UM/Evan Schneider)
Akisisitiza umuhimu wa maandalizi ya kukabiliana na majanga mkurugenzi wa FAO José Graziano da Silva. Amesema kuwajengea uwezo hususani watu wa vijijini ni muhimu saana kwani yawe mafuriko au tetemeko, kilimo kinasalia kuwa uti wa mgongo kwa mamilioni na hakikisho la uhakika wa chakula kote duniani.
image
Ertharin Cousin.(Picha:UM/Evan Schneider)
Naye mkurugenzi mtendani wa WFP Ertharin Cousin, Ushirika huo utaanza kutekelezwa baadaye mwaka huu na utatoa msaada kwa nchi 20 ili kufikia fursa ya kupata tahadhari mapema, kuwa na mipango na fedha, na mifumo ya kulinda, kutoa huduma na kufikisha misaada wakati majanga yanapozuka.