Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

#WHS na nuru ya elimu kwa watoto wakimbizi

#WHS na nuru ya elimu kwa watoto wakimbizi

Mkutano wa siku mbili wa utu wa kibinadamu ukifikia ukingoni hii leo, ahadi mbali mbali zimetolewa kuhakikisha watu milioni 130 wanapatiwa usaidizi wa kibinadamu ikiwemowatoto wakimbizi ambao kwao suala la elimu husalia ndoto wakati wa majanga. Flora Nducha na ripoti kamili.

(Taarifa ya Flora)

Wakati wa mkutano huo, kumefanyika mbinu mbali mbali bunifu za kusaidia wakati wa majanga ikiwemo uzazi salama, vifaa rahisi vya kubeba maji halikadhalika uzinduzi wa mfuko wa elimu kwa watoto wakimbizi.

Akizungumzia mfuko huo uitwao “Elimu haiwezi kusubiri” utakaochangiwa na serikali na kampuni binafsi, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu elimu, Gordon Brown amesema nuru sasa inaangazia watoto wakimbizi na hivyo mfuko huo utahakikisha kuwa..

(Sauti ya Brown)

“Elimu wakati wa majanga haisahauliki na kwamba tunaweza kutumia fedha za maendeleo kupeleka watoto shuleni.”

Kwa mujibu wa Brown, katika miezi michache iliyopita, mfuko huo umewezesha watoto wakimbizi Laki Mbili nchini Lebanon kwenda shuleni.