Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za kubana demokrasia kabla ya uchaguzi DR Congo zatia hofu:UM

Hatua za kubana demokrasia kabla ya uchaguzi DR Congo zatia hofu:UM

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , imechukua hatua kadhaa tangu Januari mwaka mwaka jana kubana demokrasia kabla ya uchaguzi mkuu.

Hayo yamesemwa na ofisi ya haki za binadamu za Umoja wa mataifa ikiorodhesha visa 216 vya ukiukaji wa haki za binadamu unaoambatana na uhuru wa kujieleza, kujumuika na kukusanyika kwa amani.

Imeongeza kuwa hatua zinazotia wasiwasi ni pamoja na kukamatwa na kuwekwa rumande kwa watu , kuingilia mikutanoo ya asasi za kiraia na upande wa upinzani na kuwanyanyasa waandamanaji.

Serikali imetakiwa kujihusisha na mazungumzo na upinzani ili kuhakikisha kila raia anakuwa na haki ya kushiriki uchaguzi kama anavyofafanua Rupert Colville msemaji wa ofisi hiyo

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

“Serikali lazima ihakikishe kwamba uhuru wa kukusanyika kwa amani , kujieleza na haki ya kushiriki masuala ya umma kwa watu wote unaheshimiwa , bila kujali ufuasi wao wa kisiasa.”