Skip to main content

Operesheni zetu Beni zinazaa matunda dhidi ya ADF- Meja Kahoko

Operesheni zetu Beni zinazaa matunda dhidi ya ADF- Meja Kahoko

Siku ya kimataifa ya ulinzi wa amani huadhimishwa tarehe 29 mwezi Mei ya kila mwaka ikilenga kukumbuka walinda amani waliopoteza maisha yao kuhakikisha amani inakuwepo duniani, lakini vilevile kuangazia wanawake na wanaume ambao wamesafiri mbali na makwao ili kutekeleza jukumu hilo adhimu.

Hii leo tunamuangazia Meja Francis Anatory Kahoko, Naibu afisa usalama kwenye kikosi cha FIB ambacho ni cha kujibu mashambulizi cha ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko DRC, MONUSCO.

Meja Kahoko anatoka Tanzania na katika mahojiano na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ameelezea kile kinachomtia moyo kufanya kazi kila siku na hapa anaanza kwa kuelezea majukumu yake.