Baraza la Usalama lakutana na Umoja wa nchi za kiarabu

21 Mei 2016

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoj a wa Mataifa wamehitimisha ziara yao huko Misri kwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa Umoja wa nchi za kiarabu kwenye mji mkuu, Cairo.

Miongoni mwa ajenda za mkutano huo ni suala la Syria na wahamiaji ambapo mmoja wa wajumbe kwenye ziara hiyo Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Liu Jieyi amesema ni mara ya kwanza katika historia kwa  pande mbili hizo zinaketi pamoja na kujadili masuala ya Mashariki ya Kati na jamii ya kimataifa kwa ujumla.

Balozi Liu amesema kimekuwa kikao hicho kikiwa na mwakilishi wa Umoja wa nchi za kiarabu Balozi Tarek al Qouni kimekuwa ni muhimu sana hasa wakati huu ambapo ulimwenguni unasaka suluhu ya mzozo mkubwa wa Syria na hivyo mazungumzo yamefanyika wakati muafaka.

Ziara hiyo imefuatia ile iliyofanywa na wajumbe wa baraza hilo nchini Somalia na Kenya ambako wamekuwa na mazungumzo na marais wa nchi hizo kwa nyakati tofauti.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter