Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Najivunia kuwa mlinda amani;Felicity- UNMIL

Najivunia kuwa mlinda amani;Felicity- UNMIL

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya walinda amani hapo Mei 29, walinda amani wa Umoja wa Mataifa sehemu mbalimbali wamekluwa wakielezea maoni yao kuhusu jukumu wanalolibeba. Leo ni zamu ya Bi Felicity Atema.

Yeye anatokea Nigeria na yuko kwenye kikosi cha watembea kwa miguu cha Nigeria kinachohudumu kwenye mpango wa Umoja wa mataifa nchini Liberia UNMIL., anasema anajivunia sana kuwa mlinda amani.

Felicity aliingia kwenye jeshi la Nigeria mwaka 20012 na kuhudumu hapo kwa miaka saba mjini Abuja. Liberia ni fursa yake ya kwanza kuhudumu nje ya nchi kwenye Umoja wa mataifa Anazungumzia uzoefu wake katika ulinzi wa amani

(SAUTI YA FELICITY)

"Uzoefu wangu kama mlinda amani ni kwamba nimekutana na watu kutoka vikosi vya nchi zingine kama Pakistan, Misri, Bangladesh nan chi zingine, najihisi vizuri na najivunia, kwa hakika sio rahisi lakini kama mwanajeshiunahitaji kutoka na kupigania amani, na kuleta amani kwa nchi zingine”