Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran kumuhukumu kwa miaka 16 mwanaharakati wa kupinga hukumu ya kifo si haki-UM

Iran kumuhukumu kwa miaka 16 mwanaharakati wa kupinga hukumu ya kifo si haki-UM

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa imesema imeshangazwa na hukumu ya kifungo ya hivi karibuni dhidi ya mwanaharakati maarufu wa Iran anayepinga hukumu ya kifo.

Nargis Mohammadi,ambaye tayari yuko jela mjini Tehran kukiuka sheria za nchi hiyo za usalama wa taifa , amekatiwa kifungo cha miaka 16 , kutokana na kazi zake za kutetea haki za binadamu.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa , imetoa wito wa kuachiliwa kwa mwanaharakati huyo ikisema imeripotiwa kwamba hapati fursa inahostahili kupewa huduma za afya anazohitaji.