Baraza la Usalama lajadili kambi ya Dadaab na rais wa Kenya
Wakiwa ziarani Afrika, wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekutana leo na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kuzungumza naye kuhusu uamuzi wake wa kufunga kambi ya wakimbizi ya Dadaab alioutangaza wiki chache zilizopita.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano huo, Mwakilishi wa kudumu wa Msiri kwenye Umoja wa Mataifa Amr Abdellatif Aboulatta amesema nuru imeanza kuonekana kuhusu suala hilo.
Ameeleza kwamba wanachama wa Baraza la Usalama wametambua mchango muhimu wa Kenya katika kuendeleza utulivu na amani kwenye ukanda huo, kupitia Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia AMISOM, hifadhi kwa malaki ya wakimbizi na hata ukuaji wa uchumi wa kitaifa ambao kwa mujibu wa Bwana Abolatta umekuwa mfano kwa ukanda mzima.
Aidha Bwana Aboulatta amesema wanachama hao wameeleza wasiwasi wao kuhusu uamuzi wa kufunga kambi ya Dadaab, wakisisitiza kwamba huenda haitaleta faida yoyote.
Akijibu suala la mwandishi wa habari kuhusu jibu lililotolewa na Rais Kenyatta kuhusu suala hilo, Bwana Aboulatta akasema
(Sauti ya Bwana Aboulatta)

Kuhusu AMISOM, wanachama wa Umoja wa Mataifa wamesema kwamba Baraza la Usalama hivi karibuni litaamua kuongeza muda wa mamlaka hiyo na kuangazia jinsi ya kuijengea uwezo zaidi.