Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNIDO na WAIPA waungana kuchagiza uwekezaji

UNIDO na WAIPA waungana kuchagiza uwekezaji

Shirika la Umoja wa mataifa la maendeleo ya viwanda UNIDO na muungano wa wa mashirika ya kimataifa ya uwekezaji WAIPA watashirikiana katika miradi ya pamoja ili kuimarisha sekta binafsi na kushiriki shughuli zenye lengo la kushagiza uwekezaji unaojumuisha wote na maendeleo endelevu ya viwanda.

Makubaliano baina yao yametiwa saini leo Ijumaa mjini Vienna na Li Yong mkurugenzi mkuu wa UNIDO na Bostjan Skalar mwenyekiti na mkurugenzi mtendani wa WAIPA.

WAIPA ni shirika lisilo la kiserikali lililojikita katika kuchagiza uwekezaji wenye lengo la kuimarisha maendeleo na uwezo wa mashirika yanayochagiza uwekezaji kote duniani. Hivi sasa ina mashirika wanachama 170 kutoka mataifa 130.

Ushirika baina ya UNIDo na WAIPA unatokana na msingi kwamba wote wanaamini kuwa uwekezaji wa moja kwa moja wan je ni chachu ya ukuaji wa uchumi na unaweza kuwa na jukumu kubwa katika maendeleo endelevu yanayojumuisha wote.

Na ushirika huu hautosaidia uwekezaji tuu bali ufikiaji wa uwekezaji endelevu utakaosaidia upatikanaji wa kazi zenye hadhi kuinua maisha ya watu.