Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwezi Aprili wavunja rekodi ya joto

Mwezi Aprili wavunja rekodi ya joto

Mwezi Aprili mwaka huu umekuwa mwezi wenye joto zaidi katika historia ya dunia, limesema leo Shirika la Hali ya Hewa WMO.

Taarifa iliyotolewa la WMO inaonyesha kwamba wastan ya halijoto ya mwezi Aprili imezidi wastan ya karne ya 20 kwa nyuzi 1.1 ya Selisiasi

Clare Nullis ni msemaji wa IOM

(Sauti ya bi Nullis)

"Joto tuliloshuhudia mwaka 2015 limegonga vichwa vya habari wakati ule, tulikuwa na wasiwasi mkubwa. Joto tunaloona mwaka 2016 linaifanya mwaka 2015 kuonekana afadhali. Sababu ya kwanza ya joto kubwa zaidi ni ongezeko la joto duniani na ,abadiliko ya tabianchi yaliyosababishwa na shughuli za binadamu."

Kwa hivyo Bi Nullis amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za mara moja ili kutekeleza makubaliano ya Paris ili kudhibiti mabadiliko ya tabianchi.