Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazingira si shwari kuanza mazungumzo ya amani ya Syria- Mwakilishi

Mazingira si shwari kuanza mazungumzo ya amani ya Syria- Mwakilishi

Nchini Syria kazi ya kufikisha misaada katika jamii zilizozingirwa ni ngumu lakini kuna matumaini kwamba hali itaimarika kutokana na shinikizo jipya la jumuiya ya kimataifa , umesema Umoja wa mataifa leo Alhamisi.

Tangazo hilo limetolewa Geneva na bwana by Jan Egeland, mratibu wa kikosi kazi cha Umoja wa mataifa kwa ajili ya masuala ya kibninadamu Syria akiwa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya taifa hilo Staffan de Mistura, ambaye amesema mazingira bado si shwari kuanza tena mazungumzo ya amani mjini Geneva.

Jumla ya miji 18 bado inazingirwa nchini Syria , lakini bwana Jan egelenda amesema kuna matumaini japo kidogo baada ya msaada kufika kwa mara ya kwanza Mashariki mwa Harasta baada ya zaidi ya miaka mitatu. Na hivyo kufanya jumla ya miji 13 ambayo inazingwa , kupata msaada wa Umoja wa mataifa na washirika wake tangu mwanzoni mwa mwaka huu.Bwana Egeland anaongeza..

(SAUTI YA EGELAND)

“Lakini huo ndio mwisho wa habari njema , kwa sababu Mei ni moja ya miezi migumu sana kwa mwaka huu. Tuliwafikia watu zaidi ya asilimi 40 mwezi uliopita wa Aprili na misaada ya kibinadamu. Mwezi huu hadi sasa labda tumewafikia asilimia 5.”

Akizitaja nchi za Urusi, Iran, Marekani na Saudia , Egeland amesema ana Imani watasaidia kupatikana kwa fursa za kufikisha misaada katika wiki zijazo. Na kuhusu mazungumzo ya amani mjini Geneva mwakilishi maalumu Staffan de Mistura amesema amedhamiria kuyaitisha tena hivi karibuni."