Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali ya ndege ya EgyptAir yaua watu 66, UM watuma rambirambi

Ajali ya ndege ya EgyptAir yaua watu 66, UM watuma rambirambi

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mogens Lykketoft ametuma salamu za rambirambi kwa serikali ya Misri na mataifa mengine ambayo yamepoteza raia wao kufuatia ajali ya ndege ya shirika la ndege la Misri, EgyptAir.

Ndege hiyo ikiwa na abiria 66 wakiwemo watoto watatu, imeanguka bahari ya Mediteranea leo wakati ikisafiri kutoka Paris, Ufaransa kwenda Cairo, Misri.

Bwana Lykketoft katika taarifa yake iliyotolewa Copenhagen anakoshiriki mkutano, ameelekeza rambirambi hizo kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki.

Kwa mujibu wa waziri wa masuala ya anga wa Misri, abiria wanatoka Misri, Ufaransa, Iraq, Uingereza, Kuwait, Saudia, Sudan, Chad , Ureno, Canada, Ubelgiji na Algeria.