Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii ya kimataifa inusuru watoto DRC: Mwenengabo

Jamii ya kimataifa inusuru watoto DRC: Mwenengabo

Jamii ya kimataifa imetakiwa kuingilia kati kunusuru watoto wanaodhulumiwa haki hata kuuawa nchini Jamhuri ya Kidemokaria ya Congo DRC. Amesema Mkurugenzi wa taasisi ya haki za watu wa asili Afrika Mashariki na kati ECAAIR Fredrick Mwenengabo.

Katika mahojiano maalumu na idhaa hii mjini New York, Marekani anakohudhuria mkutano wa jamii ya watu wa asili unaofikia tamati Ijumaa, Bwana Mwenengabo amesema kutokana na vita watoto nchini DRC wamekuwa wakikumbana na madhila yasiyolezeka.

(SAUTI MWENENGABO)

Hivyo ametaja kile taasisi yake inafanya kukomesha udhalimu kwa watoto.

(SAUTI MWENENGABO)