Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasanii watumbuiza Miami kusaidia Ecuador

Wasanii watumbuiza Miami kusaidia Ecuador

Mnamo Aprili 16, 2016, tetemeko la ardhi liliua mamia ya watu na kusababisha uharibifu mkubwa nchini Ecaudor, ukiwemo kuporomosha majengo. Kwa ujumla, tetemeko hilo la ardhi liliua zaidi ya watu 600, na kuathiri maisha ya watu wapatao milioni mbili.

Kufuatia janga hilo la kiasili, ofisi ya biashara ya Ecuador jijini Miami, katika jimbo la Florida nchini Marekani, iliandaa tamasha la muziki katika kipindi cha siku 11, likilenga kuleta pamoja wasanii mashuhuri kutoka Amerika ya Kusini, katika juhudi za kuwasaidia waathitika wa tetemeko la ardhi nchini Ecuador.

Kupitia tamasha hilo, zaidi ya dola 213, 000 zilichangishwa, kupitia uuzaji wa tikiti, zaidi ya dola 15,000 kupitia michango ya simu ya mkononi. Fedha hizo zote zitakwenda kwa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), ili liendelee kusaidia jamii zilizoathiriwa kujikwamua. Kujua mengi zaidi yaliyojiri Miami katika tamasha hilo, ungana na Assumpta Massoi katika makala hii.