Skip to main content

Niger: Mkuu wa OCHA anasisitiza mshikamano wa wadau wote katika masuala ya kibinadamu

Niger: Mkuu wa OCHA anasisitiza mshikamano wa wadau wote katika masuala ya kibinadamu

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu OCHA, Stephen O’Brien amehitimisha ziara yake nchini Niger ambapo ameshuhudia athari zinazowakumba watu waliolazimika kuhama makwao.

Taarifa iliyotolewa leo inaeleza kwamba Bwana O’Brien ametembelea eneo la Diffa ambalo ni makazi ya wakimbizi zaidi ya 240,000 waliokimbia mashambulizi ya Boko Haram. Kwenye eneo hilo, watu wawili kati ya watatu ni wakimbizi au wakimbizi wa ndani.

Bwana O’Brien amevisihi vikundi vya waasi kuhakikisha raia wanalindwa kwa mujibu wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu.

OCHA imeongeza kwamba wadau wa kibinadamu kwa ushirikiano na serikali ya Niger wanatarajia kusaidia watu wapatao milioni 2 wanaokumbwa na njaa nchini humo.

Hata hivyo Bwana O’Brien amesisitiza kwamba, wakati wa kuelekea kongamano la kimataifa la masuala la kibinadamu linalofanyika mwezi huu Istanbul, ni muhumu kuunda mpango mkakati unaohusisha masuala ya kisiasa, kimaendeleo, kimazingira na kibinadamu ili kutatua mizozo ya aina hiyo.