Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukuaji wa miji uende sanjari na ufikiaji wa SDG’s:UNHABITAT

Ukuaji wa miji uende sanjari na ufikiaji wa SDG’s:UNHABITAT

Wakati theluthi mbili ya watu duniani wanatarajiwa kuishi mijini ifikapo mwaka 2030, na miji kuzalisha asilimia 80 ya pato la taifa yaani GDP, ukuaji wa miji  ni fursa nzuri ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Makazi (UNHABITAT) iliyozinduliwa leo.

Ripoti hiyo iitwayo “Ripoti ya Miji Duniani 2016:Ukuaji na Maendeleo”  inasema ajenda mpya ya miji inahitajika ili kubadili uwezo wa miji, kwani kusipokuwa na mipango miji mizuri, ukuaji wa miji unaweza kusababisha ongezeko la kutokuwepo kwa usawa, kukuwa kwa mitaa ya mabanda na athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi. Akizungumza na idhaa hii Tom Osanjo  mwandishi na afisa mawasiliano wa UN-HABITAT amefafanua umuhimu wa ripoti hii..

(TOM CUT 1)

Na kuhusu muingiliano na SDG’s akaongeza...

(TOM CUT 2)