Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutokuwepo utashi wa kisiasa Ulaya kunasababisha madhila kwa maelfu ya wahamiaji:UM

Kutokuwepo utashi wa kisiasa Ulaya kunasababisha madhila kwa maelfu ya wahamiaji:UM

Madhila kwa wahamiaji nchini Ugiriki ni matokeo ya kutokuwepo na mtazamo wa muda mrefu na ukosefu wa utashi wa kisiasa kwa muungano wa Ulaya, amesema mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa François Crépeau akihitimisha ziara yake nchini Ugiriki.

Mtaalamu huyo wa haki za binadamu ameonya kwamba huu sio tu mtafaruku wa kibinadamu , la msingi zaidi ni mtafaruku wa kisiasa ambao Muungano wa Ulaya na nchi nyingi wanachama wa Ulaya wameitelekeza Ugiriki , nchi ambayo inajitahidi kutekeleza hatua kali kukabiliana na suala hilo linalohitaji juhudi kutoka wanachama wote.

Bwana, Crépeau amesisitiza kwamba kufungwa kwa mipaka inayoizunguka Ugiriki ukichanganya na makubaliano mapya ya Muungano wa Ulaya na Uturuki , kumeongeza wahamiaji wa kiholela nchini Ugiriki.

Tofauti na awali Ugiriki sio tena kituo cha muda, na inahangaika kukabiliana na mahitaji ya haraka ,wakati hakuna msiammo wa pamoja wa Muungano wa Ulaya kuisaidia nchini hiyo.