Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP, NAADS kujenga maghala ya nafaka, Uganda

WFP, NAADS kujenga maghala ya nafaka, Uganda

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika linalohusika na huduma za ushauri katika kilimo la serikali ya Uganda (NNADS) wamekubaliana kujenga magahala kumi ya nafaka katika wialya 10 nchini humo, katika miezi mine ijayo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kushughulikia changamoto za uhifadhi wa nafaka kote nchini. John Kibego na Taarifa zaidi.

(Taarifa ya Kibego)

Mpango huo unaolenga kuinua uwezo wa wakulima wadogo wadogo kufikia masoko bora ya nafaka, utafaidi familia 4,000 za wakulima katika wilaya za Adjumani, Hoima, Kibaale, Kiboga, Kiryandongo, Kyenjojo, Masindi, Mubende, Nakaseke and Napak.

Kulingana na mkataba ulioridhiwa na pande zote mbili, NAADS itatoa dola milioni moja kwa WFP za kuisaidia katika ujenzi huo, na kila ghala likiwa na uwezo wa kuhifadhi tani 200 za nafaka.

Michael Dunford, Mkurugenzi wa WFP, Uganda ameonyesha matumaini kuwa uwepo wa miundombinu bora utasaidia wakulima hao wadogo wadogo kufikia masoko kwa wakati mwafaka na kuepuka njaa.